MADSON LUTHERAN DISPENSARY

ELCT RUAHA DAY CARE

KKKT USHARIKA WA RUAHA

Usharika wa Ruaha unatoa huduma za afya kupitia Zahanati ya Kilutheri Madson (Madson Lutheran Dispensary) iliyopo kijiji cha Kitete Msindazi, katika Halmashauri ya wilaya ya Kilosa Mkoa wa Morogoro. Huduma zinazotolewa ni pamoja na:-

  1. Wagonjwa wa nje.
  2. Ushauri.
  • Maabara.
  1. Mapumziko.
  2. Huduma ya Mama na Mtoto.

Kazi ya ujenzi imefanyika kwa michango ya Wakristo na wakati mwingine Wadau wachache walichangia michango ili kuunga mkono jitihada hizi za ujenzi wa Zahanati. Kwa sasa tumeanza ujenzi wa jengo la Mama na Mtoto. Unaweza kuungana nasi katika kuifanya kazi hii kwa kutuma Mchango wako katika benki ya CRDB,

Akaunti namba 0152360965000;

Jina: ELCT RUAHA PROJECT DEVELOPMENT FUND.

Mungu akubariki.