KKKT USHARIKA WA RUAHA
IDARA YA E/KIKRISTO; VIJANA NA MASOMO YA JUU


Picha juu:
Vijana walioongoza Ibada Sikukuu ya Vijana July 2024.
Picha ya Chini: Viongozi wa Vijana baada ya Kikao na Mchungaji wa Usharika Tarehe 2/2/2025.
Picha ya Chini: Viongozi wa Vijana baada ya Kikao na Mchungaji wa Usharika Tarehe 2/2/2025.

KUHUSU IDARA
IDARA YA E/KIKRISTO; VIJANA NA MASOMO YA JUU
Kazi ya idara hii ni kusimamia mafundisho yahusuyo Elimu ya Kikristo katika madarasa ya Ubatizo, Kipaimara, Shule, Vyuo ili kuhakikisha Vijana katika usharika wanakua katika maadili mema yanayompendeza Mungu.
- Malengo:
- Idara hii inalenga kutoa elimu ya Kikristo kwa watoto, vijana na watu wazima. Pia inalenga kuwawezesha vijana na wanafunzi wa masomo ya juu kuwa na uhusiano mzuri na Mungu, na kuwaandaa kwa maisha ya Kikristo katika jamii.
Majukumu:
- Kufundisha elimu ya Kikristo katika shule na vyuo.
- Kuandaa na kuendesha makambi, mikutano na semina za vijana kuhusu maisha ya Kikristo.
- Kutoa mafunzo kwa vijana kuhusu maisha ya Kikristo na changamoto zinazowakabili katika jamii.
- Kuratibu programu za kujenga uwezo kwa vijana ili wawe na mchango mzuri katika Kanisa na jamii.