Our Pastors

HISTORIA NA UONGOZI WA USHARIKA

KUHUSU USHARIKA

HISTORIA YA USHARIKA

Usharika wa Ruaha ni miongoni mwa sharika za Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania – Dayosisi ya Ulanga Kilombero. Huduma za ibada hapa Ruaha zilianza tangu mwaka 1975 ambapo Ruaha ilianzishwa kuwa Mtaa chini ya Usharika wa Kilombero. Mwaka huo huo  wa 1975 ulizinduliwa rasmi kuwa Usharika na kuitwa Usharika wa Ruaha. Asili ya jina hili ni Mto Ruaha ambao unapita karibu na Usharika ulipo. Usharika unatoa huduma katika kata za Kidatu, Kidodi na Ruhembe zilizopo katika Tarafa ya Mikumi, Halmashauri ya wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro.

Kazi ya Mungu imeendelea kuimarika na usharika umeendelea kukua. Usharika wakati unaanza ulikuwa na Mitaa miwili, yaani hapa Ruaha na Kitete. Usharika uliendelea kupanua kazi ya injili kwa kufungua mitaa mipya ambayo ni mtaa wa Mhovu (sasa unaitwa mtaa wa Nazareth), mtaa wa Mzombe na mwaka 2024 umefunguliwa Mtaa wa Kristo Mfalme. Uliokuwa mtaa wa Kitete (wa Usharika wa Ruaha) sasa unaandaliwa kuwa usharika. Haya yote ni matunda ya kazi ya injili ambayo inaendelea katika usharika wa Ruaha. Tunawashukuru wote walioshiriki katika huduma hii tangu kuanzishwa kwa mtaa mwaka 1975 hadi sasa. Mungu awabariki.

WACHUNGAJI WALIOWAHI KUHUDUMU USHARIKANI

KUHUSU USHARIKA

ORODHA YA WACHUNGAJI

  1. Mwinjilisti/Shemasi Eliezer Kingwana
  2. Mchungaji Yona Chogo
  3. Mchungaji Henry Towegale
  4. Mchungaji Abel Jacob Mwambungu (Askofu Mstaafu kwa sasa)
  5. Mchungaji Mwangama
  6. Mchungaji Zabron Kyahe
  7. Mchungaji Benjamini Kyaponda Swale
  8. Mchungaji Beatus Kibandike
  9. Mchungaji Jonas Peter Mgawo
  10. Mchungaji Madson Lucas Kihwele 2005 – September 2022
  11. Mchungaji Yusuph Akimu Mbago Oktober 2022 hadi sasa
  1. Mwinjilisti Hosea Msafiri
  2. Mwinjilisti Herini Tumaini
  3. Mwinjilisti Meshaki Mbilinyi
  4. Mwinjilisti Frank Hamisi
  5. Mwinjilisti Isaya Paskali Chura
  6. Mwinjilisti Malaki Wikeji 2017 – 2019
  7. Mwinjilisti Gideon Stephan Mhalafu 2019 hadi sasa

ORODHA YA WAINJILISTI

MAAFISA WA USHARIKA

Mchg Yusuph Akimu Mbago

Mchg Yusuph Akimu Mbago

Mchungaji Kiongozi

Maria Jotham Mwanjalila

Maria Jotham Mwanjalila

Katibu M/Hazina wa Usharika

Mwinj.Gideon stephan Mhalafu

Mwinj.Gideon stephan Mhalafu

Mwinjilisti wa Usharika